Hot cakes!

Wednesday, September 14, 2011

Ajali ya meli yasababisha vifo vya mamia ya watu Zanzibar!

 Watu wasiopungua 187 wamekufa baada ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.
Msemaji wa serikali amesema watu 620 walionusurika wameokolewa. Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo.
Inadhaniwa kuwa meli hiyo ilizama baada ya injini yake kukosa nguvu.



 Shughuli za uokoaji zilikwama kwa kuwa meli hiyo ilizama usiku.




Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo, lakini watu 325 walionusurika wameokolewa, kwa mujibu wa waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar.
Meli hiyo, MV Spice Islander ilikuwa ikisafiri kati ya Kisiwa kikuu cha Unguja kuelekea Pemba.
Meli hiyo ilikuwa ikirejesha watu baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.

Mamlaka za huko zimezidiwa na tukio hilo na zimeomba msaada kutoka nje.Serikali ya Zanzibar imeunda kituo cha uokoaji na kutoa wito kwa taasisi zote kusaidia katika shughuli za uokozi. Serikali hiyo pia imeomba msaada kutoka nchi nyingine za nje, kama vile Kenya na Afrika Kusini.

Walionusurika walichukuliwa na boti za kibinafsi na kupelekwa katika bandari ya Zanzibar, amekaririwa kamishna wa polisi wa Zanzibar Mussa Hamis.

Miili ya watu imekuwa ikisukumwa katika pwani ya Zanzibar na mawimbi. Mpaka sasa miili ya watu 100 wamepatikana, amesema mwandishi wa BBC Ali Saleh akiwa Zanzibar.
 Maelfu ya ndugu na jamaa wanasubiri kusikia taarifa za ndugu zao ambao walikuwa ndani ya meli hiyo, anasema mwandishi wetu.
Mohhamed Aboud, waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar anasema watu 259 walionusurika wameokolewa lakini 40 kati yao wamejeruhiwa sana.
Boti yetu imechelewa kwa sababu wanatumia vyombo vyote vya baharini kuokoa watu


Catherine Purvis, mtalii kutoka Uingereza aliyepo Zanzibar, akisubiri boti ya kwenda Dar es Salaam amesema ameshuhudia miili ya watu wengi ikitolewa ndani ya maji.
"Nimesimama katika bandari ya Zanzibar nikiwa na watalii wengine kama 10 wa Marekani na Uingereza.
"Boti yetu imechelewa kwa sababu wanatumia vyombo vyote vya baharini kuokoa watu".
Rubani mmoja wa helikopta Kapteni Neels van Eijk alipita juu ya eneo la tukio.
"Tuliona walionusurika wakiwa wameshikilia magodoro na majokofu au chochote kile kinachoweza kuelea. Ni vigumu kusema idadi kamili, lakini naweza kusema walikuwepo zaidi ya watu 200 walionusurika ndani ya maji na miili ya watu pia," ameiambia BBC.
"Wakati huo, kulikuwa na boti chache zilizofika katika eneo hilo. Walikuwa wakitafuta walionusurika, ingawa bahari haikuwa imechafuka sana, mawimbi walikuwa makubwa, kwa hiyo ilikuwa vugumu kuona walionusurika.
"Tulirusha ndege yetu na kuziongoza boti hadi kwa watu walionusurika ili waweze kuwachukua. Kulikuwa na miili kadhaa ndaniya maji."
Meli hiyo iliondoka Unguja takriban saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki na inadhaniwa kuwa ilizama majira ya saa saba usiku.
Ilikuwa imebeba abiria wengi kiasi kwamba baadhi ya abiria waligoma kupanda, amekaririwa abiria mmoja aliyenusurika Abdullah daid,.




Mwenyezimungu zilaze mahali pema peponi roho za wote waliopoteza maisha. Pia akawe faraja na kuwatuliza wale wote waliopoteza ndugu, rafiki na jamaa zao wa karibu. 
Amina!

Sunday, August 21, 2011

Kina mama na kina Dada kulikoniiiii????

 
Katika pitapita The entertainer nimepokea malalamiko ya watu hawa. Kikubwa kilichowasibu ambacho bado ni tatizo tena tatizo sugu, ni NJAA.

Haimaanishi wanaandamana, La hasha, wapo tayari kwa kusubiri kupokea mgao wa vyakula vya msaada.Ni rahisi kwa kuwatazama lakini kuna ugumu endapo ukapata nafasi ya kuwa muhusika.

Ukiona mtu mzima analia ujue kunajambo, si bure. Hebu tafakari, wakati wewe unafikiria utapata wapi pesa uende saluni ukatengeneze nywele au utapata vipi pesa ukanunue simu uipendayo wapo wenzio hawajui kama wataiona kesho salama. Kwa hili huna budi kumshukuru mungu kwa kukufikisha hata hapo ulipo.

Saturday, August 13, 2011

Ipo wapi Tanzania ya kesho?

 

Sasa nije kwako mdau wangu. Vipi endapo suala hili lingekuhusu kwa namna moja au nyingine? Tuchukulie mfano wewe kama mzazi wa mtoto wa aina hii.......... Bac kama sio mzazi tufanye mlezi wa karibu au hata ndugu, Ikishindikana jaribu kijiweka nafasi hiyo wewe. Suala hili unalitazama kwa jicho lipi. Na hatua zipi madhubuti ungependa zichukuliwe (kama unadhani kuna lililo nje ya maadili)


Kwa pamoja tuijenge Tanzania yetu ya kesho!

Tuesday, August 2, 2011

Yaliyojiri Pale Mjengoni (on 30th July 2011)

Watu kibao walifurika
 Muheshimiwa Hakusita kutoa Burudani
 Shamra shamra za aina yake zilitanda.

 Manjonjo ya jamaa yakazidi kuufanya umati wa watu kutokujutia kupoteza pesa zao kama gharama za viingilio na matumizi mengine.


 Wasindikizaji nao hawakua nyuma bwana.....
 Raia nao wakatoa shvu kwa waliowakosha
 Tukiongozwa na raisi wetu, wote tulipendeza bwana eeeeeh!
 Si wabongo, si watasha... wote walikuwepo
 Si ndo maana nakuambia hatukubaki nyuma kimavazi???



 Sometime Ni mambo ya kawaida kabisa kupoteza network maeneo kama haya....
 Hebu niambie hapa kuna kulindana kweli? sababu hadi jamaa anaburudika loh!
 Ya kesho utaikosaaaaa....????

 
Picha zimetolewa kwenye mtandao wa Global-publisher.

Monday, August 1, 2011

Tunazitumiaje "Beach" zetu?

Mwanzoni ulikua ni utamaduni wa kizungu. Lakini baadae ikaanza kujitokeza hata miongoni mwa Watanzania. Hilo halina tatizo, basi ndugu zanguni tujiahidi kuiga yale yenye manufaa katika jamii zetu.


























Hebu watazame wakina dada hawa wa kitanzania ambao wamefika maeneo haya kwa lengo la mapumziko mafupi. 

 
















Ipo wapi busara yao endapo viungo au sehemu  za miili yao zikiwa nje bila sababu yoyote yenye manufaa kwao na kwa upande mwingine jamii inayowazunguka ina marika tofauti tofauti nikimaanisha wazee na watoto vilevile na vijana wenye kujiheshimu.

Watanzania tunaombwa kulifanyia marekebisho suala hili. Hakuna haja ya kuliwekea sheria ya kupinga hazi na uhuru wa mtu binafsi. Ni busara tu kati yetu ndio zinahitajika. Hebu tujali maadili yetu japo kwa kasi. Japokuwa tuna uhuru wa kufanya yale tunayojiamulia kufanya, basi tuangalie yapi ni mazuri na yenye kuleta manufaa tuyafanye kwa bidii.
 Huo ni mtazamo wangu, Wewe unasemaje?

Wednesday, July 27, 2011

Tanzania are you Reeeeeaaaadddddyyyyyyyyy.....................!


Ni yule yule mkali wetu
Tuliemsubiri Takriban miezi kadhaa

Hatimaye ndani ya Ardhi ya Tanzania
Jijini Dae-es Salaam. 
Natumai wakazi na wapenzi wa burudani hizi mmejipanga vilivyo kuupokea ugeni huu
 Shukrani kwa Serengeti kwa kutoa support la ainayake
Sasa 
 Ticket 15,000/=
Mlangoni 20,000/=

 Sio ya kukosa mtuwangu
Haina Majotroooooooo!

Monday, July 25, 2011

Tutakuwepo Fiesta on 31st July 2011.

Imekua ni Desturi ya Watanania haswa rika la vijana kusheherekea kwa shamrashamra burudani hizi maarufu kama Fiesta! (since 2000)
Dosari inaingia, Imani inawatoka, hofu inatanda miongoni mwa watu wa rika hili na wapenzi wa burudani hii.
Kutokana na adha ya mgao mkali wa umeme ambao ndio tatizo sugu kwa sasa nchini,


Je shirika hili la pekee la kusambaza umeme Tanzania [TANESCO] litaweza kutoa huduma bila kukatika kwa umeme katika eneo husika sikuhiyo?












Tunayaangaza Maisha yako.

Tuesday, July 19, 2011

Full Entertainments Tz

 Welcome to the blog full of a lot of funnies. created special for funny makers and all whom are interested with, lets join together and Share what we have. This is presented to you by E. Entertainment Production. (The best place for all your entertainments solutions)

Followers