Mwanzoni ulikua ni utamaduni wa kizungu. Lakini baadae ikaanza kujitokeza hata miongoni mwa Watanzania. Hilo halina tatizo, basi ndugu zanguni tujiahidi kuiga yale yenye manufaa katika jamii zetu.

Hebu watazame wakina dada hawa wa kitanzania ambao wamefika maeneo haya kwa lengo la mapumziko mafupi.
Ipo wapi busara yao endapo viungo au sehemu za miili yao zikiwa nje bila sababu yoyote yenye manufaa kwao na kwa upande mwingine jamii inayowazunguka ina marika tofauti tofauti nikimaanisha wazee na watoto vilevile na vijana wenye kujiheshimu.
Watanzania tunaombwa kulifanyia marekebisho suala hili. Hakuna haja ya kuliwekea sheria ya kupinga hazi na uhuru wa mtu binafsi. Ni busara tu kati yetu ndio zinahitajika. Hebu tujali maadili yetu japo kwa kasi. Japokuwa tuna uhuru wa kufanya yale tunayojiamulia kufanya, basi tuangalie yapi ni mazuri na yenye kuleta manufaa tuyafanye kwa bidii.
Huo ni mtazamo wangu, Wewe unasemaje?