
Katika pitapita The entertainer nimepokea malalamiko ya watu hawa. Kikubwa kilichowasibu ambacho bado ni tatizo tena tatizo sugu, ni NJAA.
Haimaanishi wanaandamana, La hasha, wapo tayari kwa kusubiri kupokea mgao wa vyakula vya msaada.Ni rahisi kwa kuwatazama lakini kuna ugumu endapo ukapata nafasi ya kuwa muhusika.
Ukiona mtu mzima analia ujue kunajambo, si bure. Hebu tafakari, wakati wewe unafikiria utapata wapi pesa uende saluni ukatengeneze nywele au utapata vipi pesa ukanunue simu uipendayo wapo wenzio hawajui kama wataiona kesho salama. Kwa hili huna budi kumshukuru mungu kwa kukufikisha hata hapo ulipo.