Hot cakes!

Sunday, August 21, 2011

Kina mama na kina Dada kulikoniiiii????

 
Katika pitapita The entertainer nimepokea malalamiko ya watu hawa. Kikubwa kilichowasibu ambacho bado ni tatizo tena tatizo sugu, ni NJAA.

Haimaanishi wanaandamana, La hasha, wapo tayari kwa kusubiri kupokea mgao wa vyakula vya msaada.Ni rahisi kwa kuwatazama lakini kuna ugumu endapo ukapata nafasi ya kuwa muhusika.

Ukiona mtu mzima analia ujue kunajambo, si bure. Hebu tafakari, wakati wewe unafikiria utapata wapi pesa uende saluni ukatengeneze nywele au utapata vipi pesa ukanunue simu uipendayo wapo wenzio hawajui kama wataiona kesho salama. Kwa hili huna budi kumshukuru mungu kwa kukufikisha hata hapo ulipo.

Saturday, August 13, 2011

Ipo wapi Tanzania ya kesho?

 

Sasa nije kwako mdau wangu. Vipi endapo suala hili lingekuhusu kwa namna moja au nyingine? Tuchukulie mfano wewe kama mzazi wa mtoto wa aina hii.......... Bac kama sio mzazi tufanye mlezi wa karibu au hata ndugu, Ikishindikana jaribu kijiweka nafasi hiyo wewe. Suala hili unalitazama kwa jicho lipi. Na hatua zipi madhubuti ungependa zichukuliwe (kama unadhani kuna lililo nje ya maadili)


Kwa pamoja tuijenge Tanzania yetu ya kesho!

Tuesday, August 2, 2011

Yaliyojiri Pale Mjengoni (on 30th July 2011)

Watu kibao walifurika
 Muheshimiwa Hakusita kutoa Burudani
 Shamra shamra za aina yake zilitanda.

 Manjonjo ya jamaa yakazidi kuufanya umati wa watu kutokujutia kupoteza pesa zao kama gharama za viingilio na matumizi mengine.


 Wasindikizaji nao hawakua nyuma bwana.....
 Raia nao wakatoa shvu kwa waliowakosha
 Tukiongozwa na raisi wetu, wote tulipendeza bwana eeeeeh!
 Si wabongo, si watasha... wote walikuwepo
 Si ndo maana nakuambia hatukubaki nyuma kimavazi???



 Sometime Ni mambo ya kawaida kabisa kupoteza network maeneo kama haya....
 Hebu niambie hapa kuna kulindana kweli? sababu hadi jamaa anaburudika loh!
 Ya kesho utaikosaaaaa....????

 
Picha zimetolewa kwenye mtandao wa Global-publisher.

Monday, August 1, 2011

Tunazitumiaje "Beach" zetu?

Mwanzoni ulikua ni utamaduni wa kizungu. Lakini baadae ikaanza kujitokeza hata miongoni mwa Watanzania. Hilo halina tatizo, basi ndugu zanguni tujiahidi kuiga yale yenye manufaa katika jamii zetu.


























Hebu watazame wakina dada hawa wa kitanzania ambao wamefika maeneo haya kwa lengo la mapumziko mafupi. 

 
















Ipo wapi busara yao endapo viungo au sehemu  za miili yao zikiwa nje bila sababu yoyote yenye manufaa kwao na kwa upande mwingine jamii inayowazunguka ina marika tofauti tofauti nikimaanisha wazee na watoto vilevile na vijana wenye kujiheshimu.

Watanzania tunaombwa kulifanyia marekebisho suala hili. Hakuna haja ya kuliwekea sheria ya kupinga hazi na uhuru wa mtu binafsi. Ni busara tu kati yetu ndio zinahitajika. Hebu tujali maadili yetu japo kwa kasi. Japokuwa tuna uhuru wa kufanya yale tunayojiamulia kufanya, basi tuangalie yapi ni mazuri na yenye kuleta manufaa tuyafanye kwa bidii.
 Huo ni mtazamo wangu, Wewe unasemaje?

Followers